3.23.2018

Umeme wa Mashariki | Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako


Mwenyezi Mungu alisema, Katika miaka yote ya kuipitia kazi na kusikiliza mahubiri, kuna watu wengine ambao wanajifahamu, na watu wengine ambao hawana ufahamu wowote kujihusu; watu wengine wanaweza kuzungumza kuhusu vitu fulani halisi, na kuwasiliana hali halisi zao wenyewe, kuingia kwao wenyewe, maendeleo yao wenyewe, dosari zao, na jinsi wanapanga kuingia ndani. Watu wengine hawawezi kuzungumza kuhusu mambo hayo kabisa, wanaweza tu kuzungumza kuhusu mafundisho ya dini, kuzungumza kuhusu masuala ya nje kama vile kazi ya nje, hali za sasa, maendeleo ya kueneza injili, lakini si chochote kuhusu kuingia thabiti katika maisha au uzoefu wao wenyewe. Hili linaonyesha kwamba bado hawajashika njia sahihi kuingia katika maisha. Mgeuzo wa tabia si badiliko katika matendo, si badiliko la nje lililobuniwa, si mgeuzo wa muda wa shauku, bali ni mgeuzo wa kweli wa tabia ambao huleta badiliko katika matendo. Mabadiliko kama hayo katika matendo ni tofauti kuliko mabadiliko katika mienendo ya nje. Mgeuzo wa tabia una maana kwamba umeelewa na umepitia ukweli, na kwamba ukweli umegeuka kuwa maisha yako. Zamani, ulifahamu ukweli kuhusu suala hili, lakini hukuweza kuchukua hatua kulihusu; kwako ukweli ulikuwa tu kama mafundisho ya dini yasiyodumu. Sasa, tabia yako imegeuka, na huelewi tu ukweli, lakini pia unatenda kulingana na ukweli. Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo ulikuwa unavipenda mno zamani; unaweza kuacha vitu ulivyokuwa radhi kufanya, mawazo yako mwenyewe, na fikira zako. Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo hukuweza kuviacha zamani. Huu ni mgeuzo wa tabia na ni mchakato wa kuigeuza tabia yako. Inasikika kuwa rahisi kabisa, lakini kwa kweli, mtu aliye katikati ya hilo lazima apitie shida nyingi, aushinde mwili wake na aache mambo ya mwili wake ambayo ni ya asili yake. Lazima pia apitie kushughulikiwa na kupogolewa, kuadibu na hukumu, na lazima apitie majaribio. Ni baada ya kupitia haya yote tu ndio mtu anaweza kuifahamu asili yake. Kuwa na ufahamu kiasi hakumaanishi kwamba anaweza kubadilika mara moja. Lazima apitie shida katika mchakato huo. Vivyo hivyo, je, unaweza kutia kitu fulani katika vitendo mara tu unapokielewa? Huwezi kukitia katika vitendo mara moja. Katika muda ambao unachukua ili uelewe, wengine watakupogoa na kukushughulikia, na mazingira yatakulazimu kukifanya kwa njia hii au njia hiyo. Wakati mwingine, watu hawako radhi kulipitia hili, wakisema, "Kwa nini nisiweze kukifanya kwa njia hiyo? Ni lazima nikifanye kwa njia hii?" Wengine husema, "Unapaswa kukifanya kwa njia hii. Kama unamwamini Mungu, basi unapaswa kukifanya kwa njia hii. Kukifanya kwa njia hii ni kwa mujibu wa ukweli." Mwishowe, watu watafikia mahali fulani ambapo wanaelewa mapenzi ya Mungu na wanafahamu ukweli fulani baada ya kupitia majaribio fulani, na watafurahia na kuwa radhi kuyafanya kwa kiasi fulani. Mwanzoni watu watasita kulifanya. Chukua mfano wa kutimiza wajibu kwa bidii. Watu wana ufahamu fulani kuhusu kutimiza wajibu wao na kuwa waaminifu kwa Mungu, na pia wanaelewa ukweli, lakini ni wakati gani watajitolea kabisa kwa Mungu? Watatimiza wajibu wao kwa jina na matendo lini? Hili litahitaji muda fulani. Wakati wa mchakato huu, huenda ukapitia shida nyingi; watu watakushughulikia, watu watakupogoa, watu watakudhibiti, watakushurutisha na watakulazimisha. Macho ya kila mtu yatakukazia, na hatimaye, utatambua: Ni tatizo langu. Je, inakubalika kutimiza wajibu wangu bila kujitolea? Siwezi kuwa mvivu na mzembe. Roho Mtakatifu anakupa nuru kutoka ndani na Atakushutumu unapofanya kosa. Wakati wa mchakato huu, utaelewa mambo mengine kukuhusu na utajua kwamba wewe ni mchafu sana, una nia nyingi sana zako mwenyewe na tamaa nyingi sana katika kutimiza wajibu wako. Baada ya wewe kulijua hili, unaweza kuishika njia sahihi polepole na utaweza kuyabadilisha matendo yako.
Kuhusu kiini cha kutimiza wajibu wenu, ni jinsi gani mnatimiza wajibu wenu vizuri kwa kweli? Ni jinsi gani mnatimiza wajibu wenu kulingana na ukweli baada ya kugeuza tabia zenu? Kwa kuyatafakari haya, unaweza kujua tabia yako imegeuzwa kiasi gani kweli. Mgeuzo wa tabia si jambo rahisi hivyo. "Matendo yangu yamebadilika, na ninafahamu ukweli. Naweza pia kuzungumza kuhusu uzoefu fulani katika kila kipengele cha ukweli na naweza kuzungumza kuhusu umaizi fulani mdogo. Zaidi ya hayo, Roho Mtakatifu amenishutumu kuhusu jambo hili na sasa naweza kuliacha kidogo na naweza kutii kidogo." Hili halihesabiki kama mgeuzo katika tabia ya maisha. Kwa nini? Unaweza kuacha kidogo, lakini unachotenda bado hakijafikia kiwango cha kutia ukweli katika vitendo kweli. Labda mazingira yako yanafaa kwa muda na hali zako zinafaa, au hali zako zinakushurutisha kutenda kwa njia hii, au hali yako ya akili ni imara na Roho Mtakatifu anafanya kazi, basi unaweza kulifanya. Kama ungekuwa katikati ya majaribio kama Ayubu ambaye alivumilia maumivu ya majaribio, au kama Petro ambaye Mungu alimwambia afe, je, ungeweza kusema, "Hata kama ningekufa baada ya kukujua, ingekuwa sawa"? Mgeuzo katika tabia haufanyiki ghafla sana, na haimaanishi kwamba unaweza kutia ukweli katika vitendo katika kila mazingira baada ya wewe kuelewa ukweli. Hii inahusisha asili ya mwanadamu. Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi walio na mienendo fulani ya nje, wanaoamini "Ninatia ukweli katika vitendo. Je, kwani sitimizi wajibu wangu? Je, sikuacha familia na kazi yangu? Je, kwani sitii ukweli katika vitendo kwa kutimiza wajibu wangu?" Lakini Mungu asema: "Sitambui kwamba unatia ukweli katika vitendo." Hii ni nini? Hii ni aina ya mwenendo. Kusema kweli, unaweza kuhukumiwa kwa hilo; halitasifiwa, halitakumbukwa. Hata kusema kweli zaidi, katika kulichangua hili, unafanya uovu, mwenendo wako unampinga Mungu. Kutoka nje, hukatizi, husumbui, huharibu chochote, au kukiuka ukweli wowote. Inaonekana kile ambacho unafanya ni chenye mantiki na cha maana, lakini unafanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kutegemea chanzo jinsi Mungu amehitaji, kuona kama kuna badiliko katika tabia yako au kama umetia ukweli katika vitendo. Haihusu kukubali mawazo na maoni ya mwanadamu, au kwa hiari zako mwenyewe. Badala yake, ni Mungu ndiye husema kama unakubali mapenzi Yake; ni Mungu ambaye husema kama matendo yako yana ukweli na kama yanafikia viwango Vyake au la. Kujipima dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo njia sahihi tu. Mgeuzo katika tabia na kutia ukweli katika vitendo si sahili na rahisi kama wanavyodhani watu. Je, mnaelewa sasa? Mna uzoefu wowote katika jambo hili? Huenda msilielewe ikiwa linahusisha kiini cha masuala. Mmeingia juujuu sana. Mnakimbia huku na huko siku nzima, tangu macheo hadi magharibi, mnarauka mapema na kukawia kwenda kulala, lakini hamwelewi waziwazi mgeuzo wa tabia ni nini au hali yake ya kweli ni nini. Je, hii si ya juujuu? Haijalishi kama ninyi ni wa zamani au wapya, huenda msihisi kiini na kina cha mgeuzo katika tabia. Mnajuaje kama Mungu anawasifu au la? Angalau zaidi, utahisi imara kwa hali isiyo ya kawaida katika moyo wako kuhusu kila kitu ambacho unafanya, utahisi Roho Mtakatifu akikuongoza na kukupa nuru na Akifanya kazi ndani yako wakati unatimiza wajibu wako, unapofanya kazi yoyote katika familia ya Mungu, au katika nyakati za kawaida; mwenendo wako utapatana na maneno ya Mungu, na unapokuwa na kiwango fulani cha uzoefu, utahisi kwamba ulichofanya zamani kilikuwa cha kufaa kiasi. Ikiwa baada ya kupata uzoefu kwa kipindi cha muda, unahisi kwamba baadhi ya vitu ambavyo ulifanya zamani havikufaa na hujaridhika navyo, na kweli hakukuwa na ukweli ndani ya vitu ulivyofanya, basi inathibitisha kwamba kila kitu ulichofanya kilikuwa kinampinga Mungu. Inathibitisha kwamba huduma yako ilikuwa imejaa uasi, upinzani na mienendo ya binadamu. Baada ya kusema hili, mnapaswa kuelewa vipi kugeuza tabia yenu? Je, mnaelewa? Huenda msijadili kwa kawaida kugeuza tabia yenu na kuwasiliana mara chache uzoefu wenu wenyewe. Katika hali bora zaidi, mnawasiliana: "Sikuwa mzuri wakati fulani uliopita. Baadaye nilimwomba Mungu, nikisema, 'Eh Mungu, nipe nuru na mwangaza.' Na, Mungu akanipa nuru, 'Ni lazima kwa wale wanaomfuata Mungu kuwa na majaribio.' Nilipotafakari hili, nilihisi kwamba lilikuwa sahihi, kwa hiyo heri nivumilie. Mwishowe nguvu zangu ziliamka, na sikuwa hasi tena. Hata hivyo, sikuwa nimetimiza wajibu wangu kwa bidii." Baada ya kuwasiliana kuhusu hali hizi, watu wengine wanasema: "Sisi sote tuko takriban sawa, sisi ni weusi kama kunguru." Ni udhia kuzungumza kuhusu mambo haya kila mara. Ikiwa mambo ya kina hayawezi kueleweka, mwishowe, hakuna mgeuzo katika tabia.
Mgeuzo katika tabia hasa huhusu mgeuzo katika asili yako. Asili si kitu unachoweza kuona kutoka kwa mienendo ya nje; asili inahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuishi kwa watu. Inahusisha moja kwa moja maadili ya maisha ya binadamu, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi, na kiini cha watu. Kama watu hawangeweza kukubali ukweli, basi hawangekuwa na migeuzo katika hali hizi. Ni kama watu wamepitia kazi ya Mungu tu na wameingia kwa ukamilifu katika ukweli, wamebadilisha maadili na mitazamo yao kuhusu kuishi na maisha, wameyatazama mambo kwa njia sawa na Mungu, na wamekuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zao zinaweza kusemekana zimebadilika. Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, huenda ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika matendo yako, na hayatoshi kuwa mgeuzo katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, na huenda ukaweza kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako, lakini Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, bado hutii, unatafuta visababu, na unaasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumlaumu Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linathibitisha kwamba bado una asili ya kumpinga Mungu na kwamba hujageuka hata kwa kiwango kidogo kabisa. Watu wengine hata humhukumu Mungu, wakisema kwamba Mungu si mwenye haki. Wana fikira kuhusu Mungu, na bado wanaweza kubishana au kumwomba Mungu: "Mungu anapaswa kufanya jambo hili waziwazi ili kila mtu alizungumzie." Matendo kama hayo yanathibitisha kwamba wao ni pepo waovu wanaompinga Mungu. Asili yao haitawahi kugeuka. Mtu wa aina hii anapaswa kusahaulika. Ni wale tu wanaoweza kukubali ukweli, wanaotafuta na kuchunguza ili kupata ukweli wakati ambapo hawaielewi kazi ya Mungu ndio wana tumaini la kupata mgeuzo katika tabia zao. Katika uzoefu wako, kuna hali nyingine za kawaida zinazohitaji kubainishwa. Labda wewe hulia kwa uchungu unapoomba, au labda wewe huhisi kiwango kikubwa cha upendo kwa Mungu ndani ya moyo wako na unahisi uko karibu na Mungu. Hii hasa ndiyo hali wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako, lakini bado humpendi Mungu, bado huna ukweli, na haiwezi kusemwa bila shaka kwamba tabia yako imegeuzwa.
Unaanzia wapi katika kugeuza tabia yako? Je, mwajua? Huanza na kufahamu asili yako mwenyewe. Hili ndilo muhimu. Basi unaanzaje kuifahamu? Watu wengine husema, "Tafuta maonyesho yako ya upotovu." Unajipeleleza vipi wakati umemaliza kutafuta? Unaweza kuipata hii wakati unatimiza wajibu wako. Na je, kama hutimizi wajibu wako? Unaweza kuipata? Unaweza kuipata wakati unaishi na familia yako au unashirikiana na watu? Unaipataje? Wengine husema, "Lazima uitafute wakati wote!" Ninyi wakongwe mmekuwa mkitenda kwa njia hii kwa miaka mingi; je, mnao ufahamu wa asili yenu sasa? Bado mna mwendo mrefu! Unasema kwamba unapaswa kuitafuta kila siku, wakati wote; mbali na kula na kulala, lazima uitafute kila mara. Unatafuta wapi? Unatafuta ndani ya vitu gani? Unaipataje? Matokeo yatakuwa yapi? Wengine husema, "Kuifahamu asili yako." Unapofahamu asili yako, unaweza kugeuka. Ni rahisi kwa mtu yeyote kusema hili. Lakini unatafuta vipi? Unaielewaje? Lazima kuwe na njia. Huwezi kuzungumza kuhusu mambo matupu. Ikiwa kuna njia, basi utajua namna ya kupitia. Bila njia, basi unaitaja tu kauli, "Sote lazima tuelewe asili zetu. Asili zetu si nzuri. Tunapofahamu asili zetu, basi tunaweza kugeuza tabia zetu." Ukishamaliza kutaja, ni kujigamba kwa maneno tu, na hakuna anayeielewa asili yake. Hii inaitwa kunena mafundisho ya dini bila njia. Je, kufanya kazi hivi si kuharibu mambo? Matokeo ya kufanya kazi kwa njia hii yatakuwa yapi? Ninyi aghalabu huwa mnaitaja kauli, "Tufahamu asili zetu! Sote lazima tumpende Mungu! Sote lazima tumtii Mungu! Sote lazima tutii na kuanguka mbele za Mungu! Sote lazima tumwabudu Mungu! Yeyote asiyempenda Mungu hakubaliki!" Kuzungumza kuhusu mafundisho haya ya dini hakuna maana na hakutatui matatizo. Hamjalifikiria suala hili. Kwa hiyo mnawezaje kufahamu? Kuifahamu asili yako ni kuchambua kina cha nafsi yako kwa kweli; ni kile kilicho katika maisha yako. Ni mantiki ya Shetani na mitazamo mingi ya Shetani ambayo ulikuwa ukiishi kulingana nayo mwanzoni, yaani, maisha ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo. Ni kwa kufichua tu mambo ya kina ya nafsi yako ndio unaweza kuifahamu nafsi yako. Unayafichua namna gani? Kwa kuyafanya mambo tu, watu wengi hawataweza kuyafichua na kuyachambua. Mara nyingi, baada ya kumaliza kufanya jambo fulani, hufikii ufahamu. Labda miaka mitatu au mitano baadaye utazinduka, na utakuwa na ufahamu fulani.
Sasa, ili kuifahamu asili yako, lazima ushirikishe vipengele kadhaa: Kwanza, lazima uelewe kile ambacho unapenda ndani ya moyo wako. Hilo halimaanishi vitu unavyopenda kula au kuvaa, bali linamaanisha aina ya vitu unavyopenda, vitu unavyohusudu, vitu unavyoabudu, vitu unavyotafuta, na vitu unavyozingatia. Je, mnalielewa hili? Je, wajua aina gani za vitu zinahusishwa katika vitu unavyopenda? Ni vitu ambavyo huwa aghalabu unavizingatia, vitu unavyoabudu, aina ya watu unaopenda kuwasiliana nao, aina ya vitu unavyopenda kufanya, na aina ya watu unaopenda mno ndani ya akili yako. Kwa mfano: Watu wengi huwapenda watu mashuhuri, watu ambao ni wa madaha katika usemi wao na sura yao, au watu ambao huzungumza kwa kufanya utani; watu wengine huwapenda watu ambao hujifanya. Hiki ni kipengele kinachohusu watu ambao wanapenda kushirikiana nao. Kuhusu kipengele cha vitu ambavyo watu hupenda, ni pamoja na kuwa radhi kufanya vitu ambavyo ni rahisi kufanya, kupenda kufanya vitu ambavyo watu wengine hufikiri ni vizuri, na vitu ambavyo watu wangesifu, wangeunga mkono, na wangesifu baada ya kuviona. Kuna sifa ya jumla kuhusu vitu ambavyo watu hupenda katika asili zao. Yaani, wanapenda vitu na watu ambao watu wengine wanavihusudu kwa sababu ya sura zao za nje, wanapenda vitu na watu wanaoonekana wazuri na wa anasa, na ambao huwafanya watu wengine kuwaabudu kwa sababu ya sura zao za nje. Vitu ambavyo watu hupenda ni vizuri, vya kung'aa, vya kupendeza, na vya fahari. Watu wote huabudu vitu hivi, na inaweza kuonekana kwamba watu hawana ukweli wowote, na hawana mfano wa mwanadamu halisi. Hakuna kiwango hata kidogo cha umuhimu katika kuabudu vitu hivi, lakini watu huvipenda vitu hivi. Machoni pa watu wasiomwamini Mungu, vitu hivi ambavyo watu huvipenda ni vizuri hasa, na wako radhi hasa kuvifuatilia. Ili kutoa mfano rahisi: Watu hasa huwaabudu waigizaji, watu maarufu au waimbaji. Kuna wafuasi wa shauku miongoni mwa wasioamini. Wao huwafuata watu maarufu, wakiwataka waweke sahihi katika vitabu vyao vyenye sahihi na kuwaachia ujumbe, au kuwasalimu na kuwakumbatia. Je, mambo haya hupatikana ndani ya mioyo ya waumini? Je, wewe huimba mara chache nyimbo za watu maarufu unaowaabudu? Au wewe mara chache huiga na kuvaa mitindo ambayo moyo wako hutamani sana? Wewe huwafanya watu hawa maarufu na mashuhuri kuwa vyombo vya ibada yako na umbo la kuabudu kwako. Hivi ni vitu vya kawaida ambavyo watu huvipenda ndani yao. Je, waumini huwa hawaviabudu vitu hivi kweli, ambavyo wasioamini huviabudu? Ndani kabisa ya moyo, wengi wa watu bado wana moyo wa kuviabudu. Unamwamini Mungu, na inaonekana kana kwamba huvifuatilii vitu hivyo waziwazi. Hata hivyo, ndani ya moyo wako bado unavihusudu vitu hivyo, na bado unavipenda vitu hivyo. Mara chache huwa unafikiri: "Bado nataka kuusikiliza muziki wao, na bado nataka kutazama vipindi vya televisheni ambavyo wanaigiza ndani. Wanaishi vipi? Wako wapi sasa hivi? Kama ningeweza kuwaona na kuwasalimu, basi hiyo ingekuwa bora zaidi, na hata kama ningekufa bado ingekuwa inastahili." Haijalishi ni nani wanayemwabudu, watu wote huvipenda vitu hivi. Labda huna nafasi au huna mazingira ya kukutana na watu hawa, vitu, au vyombo hivi; hata hivyo, vitu hivi vimo moyoni mwako. Kuvitamani sana vitu hivi ni kugaagaa matopeni pamoja na watu wa dunia; ni kile ambacho Mungu huchukia sana, hakina ukweli, hakina ubinadamu, na ni mfano wa shetani. Huu ni mfano sahili, ni kile ambacho watu hupenda ndani yao. Unaweza kuifichua asili yako kutokana na vitu unavyopenda.
Vitu ambavyo watu huvipenda vinaweza kuonekana kwa kuvaa kwao. Watu wengine wako radhi kuvaa mavazi ya ajabu, mavazi yanayowavutia wengine, mavazi ya kupendeza, au mavazi ya vioja. Wako radhi kuvibeba vitu ambavyo watu huwa hawabebi kwa kawaida, na hupenda vitu vinavyowavutia watu wa jinsia kinyume. Wao huvibeba vitu hivi na kuvaa mavazi haya, ambalo huonyesha jinsi vitu hivi viko maishani mwao na ndani kabisa ya mioyo yao. Vitu hivi wavipendavyo si vya hadhi na yenye heshima, hivyo si vitu vya mtu mwaminifu. Vitu wavipendavyo si haki na mitazamo yao inafanana na ile ya watu wa dunia. Nimekutana na watu wengine ambao mavazi, mapambo, na mitazamo yao ilikuwa sawa na ile ya watu wa dunia. Singeweza kuona ukweli wowote ndani yao. Kwa hivyo, kila unachopenda, kile unachozingatia, kile unachoabudu, kile unachohusudu, na kile unachofikiria ndani ya moyo wako kila siku vyote huwakilisha asili yako. Inatosha kuthibitisha kwamba asili yako inapenda udhalimu, na katika hali mbaya, asili yako ni mbovu na isiyotibika. Unapaswa kuichambua asili yako kwa njia hii, yaani, tazama kile unachopenda na kile unachoacha katika maisha yako. Labda wewe ni mzuri kwa mtu fulani kwa muda, lakini hili halithibitishi kwamba unampenda. Kile unachopenda sana kweli ndicho hasa kilicho katika asili yako; hata kama mifupa yako ingekuwa imevunjwa, bado ungekipenda na hungeweza kukiacha. Hili si rahisi kubadilisha. Chukua mfano wa kutafuta mwenzi. Waswahili wa Pemba hujuana kwa vilemba. Kama mwanamke angempenda mtu kwa kweli, basi watu wengine hawangeweza kuzuia. Hata kama wazazi wake wangeuvunja mguu wake, bado angetoroka na mwanamme huyo; heri angekufa na aolewe na mume huyo. Hili linawezekanaje? Ni kwa sababu hakuna anayeweza kubadilisha kile ambacho mtu anacho ndani yake kabisa. Hata kama ungeutoa moyo wake na afe, nafsi yake bado ingekipenda kitu kile kile. Hivi ndivyo vitu vya asili ya binadamu, na vinawakilisha dutu ya mtu. Vitu ambavyo watu huvipenda huwa na udhalimu fulani, vingine ni dhahiri na vingine sio; vingine ni kali na vingine sivyo; watu wengine wana kiasi, na wengine hawawezi kujidhibiti; watu wengine wanaweza kuzama ndani ya vitu vya giza, na hili linathibitisha kwamba hawana hata kiwango kidogo cha uhai. Kama watu wangeweza kutomilikiwa na kuzuiwa na vitu hivyo, ingethibitisha kwamba tabia zao zilikuwa zimegeuzwa kidogo na kwamba walikuwa na kimo kidogo. Watu wengine huelewa ukweli fulani na huhisi kwamba wana uzima na kwamba wanampenda Mungu. Kwa kweli, bado ni mapema sana, kuigeuza tabia ya mtu si jambo rahisi. Je, asili ni rahisi kufahamu? Hata kama ungeelewa kidogo, haingekuwa rahisi kubadilisha. Hii ni sehemu ngumu kwa watu. Haijalishi jinsi watu, masuala, au vitu vinabadilika karibu nawe, na haijalishi jinsi ulimwengu unaweza kugeuzwa juu chini, kama unaongozwa na ukweli ndani yako, ukweli umekita mizizi ndani yako, na maneno ya Mungu yanaongoza maisha yako, yanaongoza mambo uyapendayo, na yanaongoza uzoefu na maisha yako, basi utakuwa umegeuka kweli. Sasa hiki kinachodaiwa kuwa mgeuzo ni watu kuwa na kiasi kidogo cha ushirikiano na kiasi kidogo cha shauku na imani tu, lakini hili haliwezi kufikiriwa kuwa mgeuzo na halithibitishi kwamba watu wana uzima; ni kwa sababu tu ya hiari za watu. Kuongezea kwa kufichua vitu ambavyo watu huvipenda sana ndani ya asili zao, vipengele vingine vinavyohusiana na asili zao vinahitaji kufichuliwa pia; kwa mfano, mitazamo ya watu kuhusu vitu, mbinu na malengo ya watu katika maisha, maadili ya maisha na mitazamo kuhusu maisha ya watu, pamoja na mitazamo kuhusu vitu vyote vinavyohusiana na ukweli. Hivi ni vitu vyote vilivyo ndani kabisa ya nafsi za watu na vina uhusiano wa moja kwa moja na mgeuzo wa tabia.
Hebu tuangalie mitazamo ya maisha ya mtu aliye na nafsi potovu ni gani. Unaweza kusema anaamini "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, akiwaacha wasio na bahati kwa majaliwa yao." Watu wanaishi kwa ajili yao wenyewe, na kwa ufupi, wao ni kama nguruwe na mbwa tu; yote wanayojali ni chakula, mavazi, na kula. Maisha yao hayana kusudi lingine na hayana hata kiwango kidogo cha maana au thamani. Mitazamo ya maisha ni ile unayotegemea ili kusalia na kuishi; ni ile ambayo ni sababu yako ya kuishi, na jinsi unaishi, Hivi vyote ni dutu ya nafsi ya binadamu. Kwa kuchambua asili za watu, utaona kwamba watu wote wanampinga Mungu. Wote ni mashetani na hakuna mtu mzuri kwa kweli. Ni kwa kuchambua asili za watu tu ndio unaweza kujua kweli dutu na upotovu wa mwanadamu na kufahamu watu wanamilikiwa na nini hasa, kile watu wanakosa kweli, kile wanapaswa kujizatiti nacho, na jinsi wanapaswa kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kuweza kuchambua kweli asili za watu si rahisi. Hakutafaulu bila ukweli na uzoefu.

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni