Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Mwenyezi Mungu alisema:Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu, na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; wanamheshimu tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata wanamstahi Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli. Katika matukio wanayoyapitia wanataka chembe za ukweli, au hata miujiza fulani isiyokuwa na maana. Watu wengi hufuata tu, wanapitia njia mbaya ili tu kupokea baraka; hawataki ukweli, wala kumtii Mungu kwa kweli ili kupokea baraka za Mungu.
Maisha ya imani kwa Mungu ya watu wote hayana maana, hayana thamani, na katika imani yao mna fikira na kazi zao za kibinafsi; hawaamini katika Mungu ili kumpenda Mungu, lakini kwa ajili ya kutaka kubarikiwa. Watu wengi hutenda jinsi wapendavyo, hufanya wanachokitaka, na kutojali anachopenda Mungu, au kama wanachokifanya ni kulingana na mapenzi ya Mungu. Watu kama hao hawawezi kupata imani ya kweli, sembuse upendo wa Mungu. Kiini cha Mungu sio tu kwa mwanadamu kuamini; vilevile ni, kwa mwanadamu kupenda. Lakini wengi wa wale wanaomwamini Mungu hawana uwezo wa kugundua hii “siri.” Watu hawathubutu kumpenda Mungu, wala hawajaribu kumpenda Yeye. Hawajawahi kugundua kuwa kuna mengi sana ya kupendeza kuhusu Mungu, hawajawahi kugundua kwamba Mungu ni Mungu anayempenda mwanadamu, na kwamba ni Mungu ambaye mwanadamu anapaswa kumpenda. Upendo wa Mungu umeonyeshwa katika kazi Yake: ni baada tu ya kupitia kazi Yake ndipo wanaweza wakagundua upendo Wake, ni katika matukio wanayopitia ya hakika tu ambapo wanaweza kufahamu upendo wa Mungu. Kuna mengi ya kupendeza kumhusu Mungu, lakini bila ya kujihusisha na Yeye kwa hakika watu wengi hawana uwezo wa kuyagundua. Hivi ni kusema, kama Mungu asingefanyika mwili, watu wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, na kama wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, pia wasingeweza kupitia Kazi Yake—na kwa hivyo upendo wao kwa Mungu ungetiwa doa la uongo mwingi na mawazo. Upendo wa Mungu ulio mbinguni si halisi kama upendo wa Mungu ulio ulimwenguni, kwa kuwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliye mbinguni umejengwa katika mawazo yao, bali si kwa yale ambayo wameyaona kwa macho yao, na yale ambayo wameyapitia wao wenyewe. Mungu anapokuja ulimwenguni, watu wanaweza kuyaona matendo Yake halisi na upendo wake, na wanaweza kuona kila kitu katika matendo na tabia Zake za kawaida, ambayo ni mara elfu halisi kuliko ufahamu wa Mungu aliye mbinguni. Bila kujali ni vipi ambavyo watu wanampenda Mungu aliye mbinguni, hakuna kitu halisi kuhusu huu upendo, na umejaa mawazo ya kibinadamu. Haijalishi udogo wa upendo wao kwa Mungu aliye duniani, huu upendo ni halisi; hata kama ni kidogo, ungali ni halisi. Mungu huwafanya watu kumjua kupitia kazi halisi, na kupitia ufahamu huu Anapata upendo wao. Ni kama Petro: kama hangeishi na Yesu, haingewezekana yeye kumwabudu Yesu. Aidha, huu uaminifu ulijengwa kwenye uhusiano wake na Yesu. Ili kumfanya mwanadamu ampende, Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu na kuishi na wanadamu, na yote Anayomfanya mwanadamu kuona na kupitia ni uhalisi wa Mungu.
Mungu hutumia uhalisi na ujio wa ukweli kuwafanya watu kuwa wakamilifu; maneno ya Mungu hutimiza sehemu ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu, na hii ni kazi ya uelekezaji na kufungua njia. Hivi ni kusema, katika maneno ya Mungu lazima utafute njia ya matendo, na lazima utafute ufahamu wa maono. Kwa kuyaelewa haya mambo, mwanadamu atakuwa na njia na maono anapotenda, na kuweza kupata nuru kupitia maneno ya Mungu, ataweza kuelewa kuwa haya mambo hutoka kwa Mungu, na kuweza kutambua mengi. Baada ya kuelewa, lazima aingie katika uhalisia mara moja, na kutumia maneno ya Mungu kumridhisha Mungu katika maisha yake halisi. Mungu atakuelekeza katika mambo yote, na Atakupa njia ya matendo, na kukufanya uhisi kuwa Mungu anapendeza sana, na kukufanya uone kuwa kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako ni kwa ajili ya kukufanya uwe mkamilifu. Ukitaka kuona upendo wa Mungu, ukitaka kwa kweli kupitia katika upendo wa Mungu, hivyo ni lazima uzame katika uhalisi, ni lazima uzame katika maisha halisi, na kuona kwamba kila kitu afanyacho Mungu ni upendo, na wokovu, na kwamba watu waweze kuacha kile ambacho si safi, na kwa ajili ya kusafisha mambo ndani yao ambayo hayana uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Mungu hutumia maneno kumkimu mwanadamu na wakati huo huo kutengeneza mazingira katika maisha halisi ambayo huwaruhusu watu kupitia, na kama watu watakula na kunywa maneno mengi ya Mungu, basi wanapoyaweka katika vitendo, wanaweza kutatua matatizo yote katika maisha yao kwa kutumia maneno mengi ya Mungu. Hivi ni kusema, lazima uwe na maneno ya Mungu ili kuzama katika uhalisi; kama huli na hunywi maneno ya Mungu, na huna kazi ya Mungu, basi hutakuwa na njia katika maisha halisi. Kama hujawahi kushiriki maneno ya Mungu, basi utashangaa wakati mambo yatakapokutokea. Unajua kumpenda Mungu pekee, na huwezi kutofautisha chochote, na huna njia ya vitendo; umevurugika na kuchanganyikiwa, na mara nyingine unaamini kuwa kwa kuuridhisha mwili unamridhisha Mungu—yote ambayo ni matokeo ya kutokula na kunywa maneno ya Mungu. Hivi ni kusema, kama huna usaidizi wa maneno ya Mungu, na kutapatapa tu katika uhalisi, basi kimsingi huna uwezo wa kupata njia ya vitendo. Watu kama hawa hawaelewi maana ya kumwamini Mungu, au hata kuelewa kumpenda Mungu kunamaanisha nini. Ikiwa, kwa kutumia nuru na uelekezaji wa maneno ya Mungu, unaomba mara kwa mara, na kuchunguza, na kutafuta, ambayo kwayo unagundua kile unachofaa kuweka katika vitendo, kutafuta fursa ya Kazi ya Roho Mtakatifu, unashirikiana na Mungu kwa kweli, na huvurugiki na kuchanganyikiwa, basi utakuwa na njia katika maisha halisi, na kumridhisha Mungu kwa kweli. Ukimridhisha Mungu, ndani yako kutakuwa na uelekezaji wa Mungu, na hasa kubarikiwa na Mungu, ambako kutakupa hisia za furaha: utahisi hasa umeheshimika kwa kuwa umemridhisha Mungu, na utahisi umeng'aa kwa ndani, na katika moyo wako utakuwa wazi na mwenye amani, dhamiri yako itafarijiwa na haitakuwa na shutuma, utahisi furaha ndani yako uwaonapo ndugu na dada zako. Hii ndio maana ya kufurahia upendo wa Mungu, na kwa kweli huku ndiko kumfurahia Mungu. Furaha ya watu kutokana na upendo wa Mungu inapatikana kwa kupitia matukio: kwa kupitia matatizo, na kupitia uwekaji ukweli katika vitendo, wanapata baraka za Mungu. Kama unasema tu Mungu anakupenda, kuwa Mungu amelipa gharama kubwa kwa watu, kuwa Mungu ameongea maneno mengi kwa uvumilivu na huruma, na Huokoa watu kila mara, utamkaji wako wa maneno haya ni upande mmoja tu wa kumfurahia Mungu. Kufurahia kwa kweli zaidi kungekuwa ni kwa watu kuweka ukweli katika vitendo katika maisha yako halisi, ambapo baadaye watakuwa na amani na kuwa wazi moyoni mwao, watahisi wakiwa wamesisimka, ndani yao, na kuwa Mungu anapendeza sana. Utahisi kuwa gharama uliyoilipa inafaa sana. Baada ya kulipa gharama kubwa katika juhudi zako, utang'aa hasa ndani yako: utahisi kuwa unafurahia upendo wa Mungu kwa kweli, na kuelewa kuwa Mungu amefanya Kazi ya kuwaokoa watu, kuwa kuwasafisha watu ni kwa ajili ya kuwatakasa, na kuwa Mungu anawajaribu watu ili kupima kama wanampenda kwa kweli. Kama utaweka ukweli katika vitendo kwa njia hii, basi hatua kwa hatua utakuza ufahamu wazi zaidi wa kazi ya Mungu, na wakati huo utakuwa unahisi kuwa maneno ya Mungu mbele yako yatakuwa wazi kabisa. Kama unaweza kuelewa waziwazi ukweli mwingi, utahisi kuwa maswala yote ni rahisi kuweka katika vitendo, kuwa utashinda swala hili, na kushinda jaribio hilo, na utaona kuwa hakuna chochote kigumu kwako, ambacho kitakufanya kuwa mtu huru na aliyekombolewa. Kufikia hapa utakuwa ukifurahia upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu wa kweli utakuwa umekushukia. Mungu hubariki wale ambao wana maono, ambao wana ukweli, ambao wana ufahamu, na ambao wanampenda kwa kweli. Watu wakitaka kuuona upendo wa Mungu, lazima waweke ukweli katika vitendo katika maisha halisi, lazima wawe tayari kuvumilia mateso na kuacha hicho wanachokipenda na kumridhisha Mungu, mbali na machozi kwenye macho yao, lazima waweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki, na ukivumilia matatizo kama haya, yatafuatiwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kwa maisha halisi, na kutokana na kupitia maneno ya Mungu, watu wanaweza kuona upendo wa Mungu, na wanaweza kumpenda Mungu kwa ukweli ikiwa tu wameuonja upendo wa Mungu.
Kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na ukweli; kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na upendo wa Mungu; na kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyobarikiwa na Mungu. Kama utatenda kwa njia hii kila mara, utauona upendo wa Mungu ndani yako hatua kwa hatua, na utamjua Mungu kama Petro alivyomjua Mungu: Petro alisema kuwa si kuwa Mungu ana busara ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo pekee, lakini, aidha, kuwa Ana busara ya kufanya kazi halisi ndani ya watu. Petro alisema kuwa Mungu hastahili tu upendo wa watu kwa sababu ya uumbaji Wake wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, lakini, vilevile, kwa sababu ya uwezo Wake wa kuumba mwanadamu, kumwokoa, kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na kutoa upendo wake kwa mwanadamu. Petro alimwambia Yesu: "Je, Hustahili upendo wa watu zaidi ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo? Kuna mengi ndani Yako ambayo yanapendeka, unatenda na kuendelea katika maisha halisi, Roho Wako ananigusa ndani, unanifundisha nidhamu, unanikemea—haya mambo yanastahili zaidi upendo wa watu." Kama unataka kuona na kupitia upendo wa Mungu, basi lazima uzuru na kutafuta katika maisha halisi, na uwe tayari kuweka kando mwili wako. Lazima ufanye azimio hili: kuwa mtu mwenye uamuzi, ambaye anaweza kumridhisha Mungu katika mambo yote, bila ya kuzembea, au kutamani kuufurahisha mwili, kutoishi kwa ajili ya mwili lakini kuishi kwa ajili ya Mungu. Kunaweza kuwa na nyakati ambazo hukumridhisha Mungu. Hii ni kwa sababu huelewi mapenzi ya Mungu; wakati ujao, hata kama itahitaji juhudi zaidi, lazima umridhishe Mungu, na lazima usiuridhishe mwili. Unapopitia kwa njia hii, utakuja kumjua Mungu. Utaona kuwa Mungu aliumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, na Amekuwa mwili ili watu wamwone kwa uhakika, na kujihusisha na Yeye, kuwa ana uwezo wa kuishi miongoni mwa wanadamu, kuwa Roho Wake aweza kufanya watu kuwa wakamilifu katika maisha halisi, kuwawezesha kuona upendo na uzoefu wa nidhamu Yake, kurudi Kwake, na baraka Zake. Kama huwa unapitia kwa njia hii, katika maisha halisi hutatenganishwa na Mungu, na kama siku moja uhusiano wako na Mungu utaacha kuwa wa kawaida, utaweza kupatwa na aibu, na kuweza kuhisi huzuni. Unapokuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutatamani kamwe kutaka kumuacha, na siku moja Mungu akisema Atakuacha, utaogopa, na kusema kuwa ni heri ufe kuliko kuachwa na Mungu. Punde tu unapokuwa na hisia hizi, utahisi kuwa hakuna uwezo wa kumwacha Mungu, na kwa njia hii utakuwa na msingi, na utafurahia upendo wa Mungu wa kweli.
Mara nyingi watu husema kuwa wamemfanya Mungu kuwa maisha yao, lakini bado wangali kupitia hatua hii. Wanasema tu kuwa Mungu ndiye maisha yao, kuwa Anawaongoza kila siku, kuwa wanakula na kunywa maneno Yake kila siku, na kuwa wanamwomba kila siku, na hivyo Amekuwa ndiye maisha yao. Ufahamu wa wanaosema hili ni wa juu juu. Ndani ya watu wengi hakuna msingi; maneno ya Mungu yamepandwa ndani yao, lakini bado hayajaota, au hata kuzaa tunda lolote. Hadi leo, umepitia uzoefu wa kiwango gani? Ni saa hii, baada ya Mungu kukulazimisha kuja umbali huu, ndio unahisi kuwa huwezi kumuacha Mungu. Siku moja ukishakuwa na uzoefu hadi kiwango fulani, Mungu akitaka kukuacha, hutaweza kufanya hivyo. Daima utahisi kuwa huwezi kuishi bila Mungu ndani yako; waweza kuwa bila mume, mke, au watoto, bila familia, bila mama au baba, bila kufurahia kwa mwili, lakini huwezi kuishi bila Mungu. Kuwa bila Mungu itakuwa kama kupoteza uhai wako, hutaweza kuishi bila Mungu. Unapopitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefanikisha imani yako kwa Mungu, na kwa njia hii Mungu atakuwa maisha yako, atakuwa msingi wa kuishi kwako, na hutaweza tena kumuacha Mungu. Unapokuwa umepitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefurahia upendo wa Mungu kwelikweli, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu mno, Mungu atakuwa maisha yako, upendo wako, na wakati huo utaomba kwa Mungu na kusema: Ee Mungu! Siwezi kukuacha, wewe ndiwe maisha yangu, naweza kuishi bila vitu vingine vyote—lakini bila Wewe siwezi kuendelea kuishi. Hiki ni kimo halisi cha watu; ni maisha halisi. Watu wengine wamelazimika kufika walipo siku ya leo: lazima waendelee wapende wasipende, na daima huhisi kuwa wako katika hali ngumu. Lazima ugundue kuwa Mungu yupo maishani mwako, kiasi kwamba kama Mungu angekuondoa kutoka katika upendo huo itakuwa kama umepoteza uhai wako; Mungu lazima awe maisha yako, na lazima uwe huwezi kumwacha. Kwa njia hii utakuwa umekutana na Mungu, na kwa wakati huu, unapompenda Mungu tena, utampenda Mungu kwa kweli, na utakuwa upendo wa kipekee, upendo safi. Siku moja matukio unayopitia yatakapokuwa kwamba maisha yako yamefikia kiwango fulani, utamwomba Mungu, utakula na kunywa maneno ya Mungu, na hutaweza kumwacha Mungu ndani, na hata kama ungetaka, hutaweza kumsahau. Mungu atakuwa maisha yako, waweza kuusahau ulimwengu, waweza kumsahau mkeo na watoto, lakini itakuwia vigumu kumsahau Mungu—hilo haliwezekani, haya ndiyo maisha yako halisi, na upendo wako wa ukweli kwa Mungu. Upendo wa watu kwa Mungu ufikiapo kiwango fulani, hakuna chochote wanachokipenda kinachoweza kulinganishwa na upendo wao kwa Mungu, Yeye ndiye mpenzi wao wa kwanza, na hivi ndivyo wanaweza kuacha vitu vingine vyote, na wawe tayari kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Unapopata pendo kutoka kwa Mungu ambalo linazidi mengine yote, utaishi katika uhalisi, na katika upendo wa Mungu.
Punde tu Mungu anapokuwa uzima katika watu, wanakuwa hawana uwezo wa kumwacha Mungu. Je, hili sio tukio la Mungu? Hakuna ushuhuda mkubwa kuliko huu! Mungu amefanya kazi hadi kiwango fulani; Amewataka watu kutoa huduma, na kuadibiwa, au kufa, na watu hawajarudi nyuma, ambalo linaonyesha kuwa watu hawa wameshindwa na Mungu. Watu ambao wana ukweli ni wale ambao, katika matukio wanayopitia ya kweli, wanaweza kusimama imara katika ushuhuda wao, kusimama imara katika nafasi zao, kusimama katika upande wa Mungu, bila kurudi nyuma, na ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wanaompenda Mungu, wale ambao, mambo yakishawatokea, wanaweza kumtii Mungu kabisa, na wanaweza kumtii Mungu hadi kifo. Matendo na ufunuo wako katika maisha halisi ndio ushuhuda wa Mungu, ni kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mwanadamu na ushuhuda wa Mungu, na huku ni kufurahia upendo wa Mungu; unapopitia hadi kiwango hiki, matukio unayopitia yatakuwa yamekuwa na athari. Watu ambao wameuona upendo wa Mungu kwa kweli ni wale ambao wanaishi kwa kudhihirisha kwa kweli, ambao kila matendo yao yanapongezwa na wengine, ambao sura yao haipendezi lakini wanaoishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu wa hali ya juu, ambao wanawasiliana kwa karibu maneno ya Mungu na huelekezwa na Mungu, na kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambao huweza kuongea mapenzi ya Mungu katika maneno yao, na wanawasiliana kwa karibu uhalisi, ambao huelewa zaidi kuhusu kuhudumu katika Roho, wanaongea kwa wazi, ambao ni wenye heshima na kuaminika, ambao hawakabiliki na wana tabia nzuri, ambao wanaweza kutii mipango ya Mungu na kusimama imara katika ushuhuda wakati mambo yanapowatokea, ambao wana utulivu bila kujali wanachokumbana nacho. Watu wengine wangali wachanga, lakini wanatenda kama mtu mzima; wamekomaa, wana ukweli, wanapendwa na wengine—na hawa ndio watu ambao wana ushuhuda, na ndio udhihirisho wa Mungu. Ni sawa na kusema, wanapopitia mambo na kufikia kiwango fulani, ndani yao watakuwa na ufahamu juu ya Mungu, tabia zao za ndani zitakuwa zimeimarika. Watu wengi hawaweki ukweli katika vitendo, na wengi hawasimami imara kwa ushuhuda wao. Ndani ya watu kama hao hakuna upendo wa Mungu, au ushuhuda kwa Mungu, na hawa ndio watu ambao wanachukiwa sana na Mungu. Wanakula na kunywa maneno ya Mungu, lakini wanachoonyesha ni Shetani, na wanaruhusu maneno ya Mungu kukashifiwa na Shetani. Ndani ya watu hawa hakuna dalili ya upendo wa Mungu, wanachokidhihirisha ni cha shetani. Kama moyo wako uko na amani na Mungu kila wakati, na huwa uko makini kwa watu na vitu vinavyokuzunguka, na kinachoendelea katika mazingira yako, na unafahamu mzigo wa Mungu, na kila mara una moyo unaomheshimu Mungu, basi Mungu atakupa nuru ndani yako. Kanisani kuna watu ambao ni "wasimamizi", wanatazama makosa ya wengine, kisha kunakili na kuwa kama wao. Hawana uwezo wa kutofautisha, hawachukii dhambi, hawachukii au kughadhibishwa na vitu vya Shetani. Watu kama hao wamejawa na vitu vya Shetani, na hatimaye wataachwa na Mungu kabisa. Wale ambao wana maono kama msingi wao, na ambao huandama maendeleo, ni wale ambao mioyo yao daima inamheshimu Mungu, ambao ni wa wastani katika maneno na vitendo vyao, ambao wasingetaka kumpinga Mungu, kumkasirisha Mungu, au Kazi ya Mungu kwao isiwe na thamani, au shida walizozipitia ziwe bure, au yale yote ambayo wameweka katika vitendo yapite bure. Ni watu ambao wako tayari kutoa juhudi zaidi na upendo wa Mungu katika njia iliyo mbele.
Watu wakimwamini Mungu, na kupitia maneno ya Mungu, kwa moyo unaomheshimu Mungu, basi ndani ya watu hao kunaweza kuonekana wokovu wa Mungu, na upendo wa Mungu. Watu hawa wana uwezo wa kumshuhudia Mungu, wanaishi kwa kudhihirisha ukweli, na kile wanachokikiri ni kweli, kile Mungu Alicho, na tabia ya Mungu, na wanaishi Kati ya upendo wa Mungu na wameona upendo wa Mungu. Watu wakitaka kumpenda Mungu, lazima wauonje upendo wa Mungu, na kuuona upendo wa Mungu; hapo tu ndipo wanaweza kupata kuamshiwa moyo ndani yao ambao unampenda Mungu, moyo ambao uko tayari kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa heshima. Mungu hawafanyi watu kumpenda kupitia maneno na sura, au kwa mawazo yao, na Hawalazimishi watu kumpenda. Badala yake, Anawafanya wampende kwa hiari yao, na huwafanya kuyaona mapenzi Yake katika kazi Yake na matamshi, ambapo baadaye wanakuwa na upendo wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio watu wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Watu hawampendi Mungu kwa sababu wameombwa na wengine kufanya vile, wala si msukumo wa hisia wa muda mfupi. Wanampenda Mungu kwa sababu wameuona upendo wake, na wameona kuwa kuna mengi kumhusu ambayo yanastahili upendo wao, kwa sababu wameona wokovu wa Mungu, busara, na matendo ya ajabu—na kutokana na hayo, wanamsifu Mungu kwa kweli, na kumtamani kwa kweli, na wanaamshiwa msisimko ndani yao kwamba hawawezi kuishi bila kumpata Mungu. Sababu ya wale ambao humshuhudia Mungu wanaweza kumtolea ushuhuda wa kufana ni kwa kuwa ushuhuda wao umekitwa kwenye msingi wa ufahamu wa kweli pamoja na matamanio ya kweli kwa Mungu, si kutokana na msukumo wa hisia, lakini kulingana na ufahamu wa Mungu na tabia Zake. Kwa sababu wamepata kumjua Mungu, wanahisi kwamba lazima wamshuhudie Mungu, na kuwafanya wale wote wamtamanio Mungu wamjue Mungu, na kufahamu upendo wa Mungu, na uhalisi Wake. Sawa na mapenzi ya watu kwa Mungu, ushuhuda wao ni wa hiari, ni halisi, na una umuhimu halisi na thamani. Si baridi, au tupu na usiokuwa na maana. Sababu ya wale tu wanaompenda Mungu kweli kuwa na thamani na maana katika maisha yao, na kuamini katika Mungu tu, ni kwa sababu watu hawa wanaishi katika mwangaza wa Mungu, na wanaweza kuishi kwa ajili ya kazi ya Mungu na usimamizi Wake; hawaishi gizani, bali wanaishi katika mwangaza; hawaishi maisha yasiokuwa na maana, ila wanaishi maisha ambayo yamebarikiwa na Mungu. Ni wale tu ambao wanampenda Mungu wanaweza kumshuhudia Mungu, ndio tu mashahidi wa Mungu, ndio tu wamebarikiwa na Mungu, na ndio tu wanaweza kupokea ahadi za Mungu. Wanaompenda Mungu ni wandani wa Mungu, ndio watu ambao wamependwa na Mungu, na wanaweza kufurahia baraka pamoja na Mungu. Ni watu hawa tu ambao wataishi milele, na ni wao tu wataishi milele katika utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mungu yuko kwa ajili ya kupendwa na watu, na anastahili upendo wa watu wote, lakini si watu wote ambao wanaweza kumpenda Mungu, na si watu wote wanaweza kumshuhudia Mungu na kushiriki mamlaka pamoja na Mungu. Kwa sababu wanaweza kumshuhudia Mungu, na kutoa juhudi zao zote kwa kazi ya Mungu, wanaompenda Mungu kwa kweli wanaweza kutembea mahala popote chini ya mbingu bila ya mtu yeyote kujaribu kuwapinga, na wanaweza kushika mamlaka na kutawala watu wote wa Mungu. Hawa watu wanakusanyika pamoja kutoka pembe zote za dunia, wanazungumza lugha tofauti na ni wa rangi tofauti, lakini kuishi kwao kuna maana sawa, wote wana moyo unaompenda Mungu, wote wana ushuhuda sawa, na wana maazimio sawa, na mapenzi sawa. Wale ambao wanampenda Mungu wanaweza kutembea ulimwenguni kote wakiwa huru, wanaomshuhudia Mungu wanaweza kusafiri duniani kote. Watu hawa wamependwa wa Mungu, wamebarikiwa na Mungu, na wataishi milele katika mwangaza Wake.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Masomo yanayohusiana Umeme wa Mashariki
Kujua zaidi Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni