2.02.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Mungu

Njia... (8)


Mwenyezi Mungu alisema, Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Biblia

Njia… (7)


Mwenyezi Mungu alisema, Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii. Hivyo, imetayarishiwa hasa sisi, na haijalishi ikiwa tutapokea baraka au kupata taabu, hakuna mwingine anayeweza kutembea njia hii.

2.01.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, ukweli

Njia... (6)


Mwenyezi Mungu alisema, Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake. Kwa hiyo mpaka leo Sijaweza kuueleza kwa dhahiri—ni kama kwamba ni kitendawili kisichofumbuliwa. Lakini kwa jumla, kundi hili letu limejaaliwa na Mungu, na Ninaendelea kuamini kwamba Mungu ana kazi nyingine ndani yetu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu

Njia… (5)


Mwenyezi Mungu alisema, Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu.

1.31.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Njia… (4)


Mwenyezi Mungu alisema, Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Yesu

Njia… (3)


MwenyeziMungu alisema, Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu! Roho Wako aliye mbinguni awape neema watu walio duniani ili moyo Wangu uweze kukugeukia Wewe kikamilifu, kwamba Roho Yangu iweze kusisimuliwa Nawe, na kwamba Niweze kuona kupendeza Kwako ndani ya moyo Wangu na Roho Yangu, ili wale walio duniani wabarikiwe kuuona uzuri Wako.

1.30.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, ukweli

Njia… (2)


Mwenyezi Mungu alisema, Labda ndugu na dada zetu wana muhtasari kidogo wa utaratibu, hatua, na mbinu za kazi ya Mungu katika China bara, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba ni heri kuwa na kumbukumbu au muhtasari kidogo wa ndugu na dada zetu. Ninatumia tu nafasi hii kusema machache ya kile kilicho moyoni Mwangu; Sizungumzi juu ya chochote nje ya kazi hii. Natarajia kwamba ndugu na dada wanaweza kuelewa hali ya moyo Wangu, na pia Naomba kwa unyenyekevu kwamba wote wanaosoma maneno Yangu wafahamu na kusamehe kimo Changu kidogo, kwamba uzoefu Wangu wa maisha kweli si wa kutosha, na kwamba kweli Siwezi kuwa na ujasiri mbele ya Mungu. Kwa hali yoyote, Mimi huhisi kila mara kwamba hizi ni sababu halisi tu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Kanisa

Njia… (1)


Mwenyezi Mungu alisema, Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi ataenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao. Lakini kilicho tofauti nayo ni kwamba leo sisi, kundi hili la watu, tunateseka kwa ajili ya neno la Mungu. Yaani, kama mtu anayemtumikia Mungu, amekutana na vipingamizi katika njia ya kuamini katika Yeye, na hii ni njia ambayo waumini wote hufuata na ni njia iliyo chini ya miguu yetu yote.

1.29.2018

Neno la Mungu | Sura ya 11

Sura ya 11


Mwenyezi Mungu alisema, Kwa macho ya mwanadamu, inaonekana hakuna badiliko katika matamshi ya Mungu wakati wa kipindi hiki, ambalo ni kwa sababu watu hawawezi kuelewa sheria ambazo kwazo Mungu hunena, na hawafahamu muktadha wa maneno Yake. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu hawaamini kwamba kuna mafumbo yoyote mapya katika maneno haya; hivyo, hawawezi kuishi maisha yaliyo mapya kiajabu, na badala yake huishi maisha yaliyokwama na yasiyokuwa na uhai. Lakini katika matamshi ya Mungu, tunaona kwamba kuna kiwango cha kina cha maana, kile kisichofahamika na pia kisichofikika na mwanadamu. Leo, kwa mwanadamu kubahatika vya kutosha kusoma maneno kama hayo ya Mungu ni baraka kuu zaidi ya zote. 

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) 

MwenyeziMungu alisema, Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu.  

1.28.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)



Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

 MwenyeziMungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu. Ni kupitia tu kwa mawasiliano ya Mungu ya kipengele hiki cha ukweli ndipo ninaona sasa kwamba uhai wa vitu vyote unapewa na Mungu, kwamba Mungu anatengeneza sheria hizi, na kwamba Anavilea vitu vyote.