11.20.2017

5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa


Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mungu mwenye mwili Amekamilisha kazi ya "ujio wa siri wa Mwana wa Adamu" Aliyetabiriwa katika Biblia, na hivi karibuni Ataonekana kwa umma katika kila taifa na sehemu ulimwenguni.

11.18.2017

Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)



Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)


       Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba "Biblia ni ufunuo wa Mungu," "Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu."

11.17.2017

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya.

11.16.2017

1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sehemu ya Pili

……Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu.

11.15.2017

1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sehemu ya Kwanza
Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo - na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. 

11.14.2017

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA: MHALIFU NI NANI?(Ukuzaji)

     Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. 

11.13.2017

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,

Kanisa la Mwenyezi MunguKatika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru.

11.11.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Mwenyezi Mungu alisema: Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani.

11.10.2017

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

kumwamini Mungu, ukweli , hukumu

 Mwenyezi Mungu alisema: Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye? Je, unajua Anachofanyia kazi kwako kila siku?

11.07.2017

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kristo, Mungu, kupata mwili

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni.

11.06.2017

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?

ukombozi, Video za Injili, Yesu Kristo

     Mwenyezi Mungu alisema,  Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno.