Sehemu ya Pili
……Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu.
Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na wanyonge.Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kuchukuliwa kwenda mbinguni baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu… kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, daima tunafurahia ugavi wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili , akielezea sauti ya moyo wake, bila kuzingatia kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunajifunza haki ya Mungu na adhama ya tabia Yake, na kufurahia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua asili na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa kwenye mikononi Yake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho yake na kufurahia upendo wake na huba yake; wakati mwingine sisi ni kama adui wake, waliofanywa majivu na ghadhabu yake katika macho yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, anatudharau, yeye hutuinua, yeye hutufariji na kutuhimiza, yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana sana, mengi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambayo yanaweza kunyakua nafasi ya mungu katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum wa huyu mwanadamu na hadhi kwa kusita pekee. Kama Yeye haneni na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu, na kuwa Yeye yumo karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu.
Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya na kutuelekeza tutakachofanya na kueleza sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuwa na hamu ya sauti ya moyo wa huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Utu kama huu na umiliki Wake haupo kwa upeo wa binadamu wa kawaida, na hauwezi kumilikiwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu ama kiini chetu, ama kuhukumu uasi wetu na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yametoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana utumwa wa shetani ama upotovu wa tabia yetu potovu Yeye huwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu, yote ambayo huelekezwa kwa mwanadamu. Ameanza enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na ametuletea matumaini, na akamaliza maisha ambayo si dhahiri, na akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na kwa muda amekuwa akikataliwa na sisi—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye Kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye kweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, na kuona nuru, na kusimamisha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso wake, na tumeona barabara iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno lake, na tunasujudu, kabisa, mbele yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila yake, na kulipa upendo wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio yake, na kushirikiana na kazi yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile anachotuaminia.
Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.
Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafunuliwa kwa neno lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani, na hata kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanakufa, na kamwe hatuwezi kumpa madai yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu kupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na kwamba hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea na barabara iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kumpata na kumtambua Yesu Kristo. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna ghadhabu ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kueleza mioyo yetu mbele yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na kuwa na hisia ya hasara kuliko vile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza kwamba sisi tunateseka kwa kupata shida kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake vimetuwezesha kwa ukweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia kwake kwa makosa ya binadamu, ikilinganishwa na ambavyo sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi. Hukumu Yake na kuadibu vimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza, jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hawezi kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kamwe tusichukiwe Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake vimetufanya tufurahie kutii neno Lake, na hatumo tayari kamwe kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine, zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.... Mwenyezi Mungu ametutamalaki, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui zake!
Sisi ni kundi la watu wa kawaida waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa kumeshindwa na Yeye. Tumepokea maisha na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu tu!
Upendo wa Mungu unazidi kuenea kama maji ya chemichemi, na wewe unapewa, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.
Kama vile daima mwezi hufuata jua, kazi ya Mungu haiishi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.
Ilielezewa Machi 23, 2010
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni