12.10.2018

Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Nyimbo

Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

I
Umeona ndani ya moyo wangu, kiburi kilichoje ndani yangu.
Nafikiri kuwa mimi ni mzuri sana na kila kitu ni duni kwangu.
Mkuu na mwenye majivuno, asili yangu ni ngumu kutupa.
Zaidi ya kudharau, mimi ni mdogo. Binadamu wamepotea. Oo, binadamu wamepotea. 
Maneno Yako yanauyeyusha moyo wangu. Mbele Yako nimekuja.
Niruhusu niishi kwa maneno Yako,
nitembee katika njia ing’aayo ya maisha, katika njia ing’aayo ya maisha.
II
Ninajifanya kuwa halisi. Je, utakosaje kuhuzunika?
Umeung’amua moyo wangu. Maneno Yako yameifunua aibu yangu.
Nikiwa na aibu kuuona uso Wako. Ni vigumu kusema kile kinachoumiza.
Nimekufuata kwa muda mrefu, bila kujali moyo Wako.
Oo, bila kujali moyo Wako.
Maneno Yako yanauyeyusha moyo wangu. Mbele Yako nimekuja.
Niruhusu niishi kwa maneno Yako,
nitembee katika njia ing’aayo ya maisha, katika njia ing’aayo ya maisha.
III
Nikijihami kwa maneno ya mafundisho, tabia haijabadilika.
Maneno Yako yamefanya mambo yawe wazi. Ni mimi nisiyetafuta.
Mtazamo wangu wenye tamaa nimeonyesha, lakini kwa ajili ya hilo Ulikuwa umenichukia.
Kwako siwezi kuasi. Dhamiri yangu lazima iwe nyoofu.
Oo, dhamiri yangu lazima iwe nyoofu.
Maneno Yako yanauyeyusha moyo wangu. Mbele Yako nimekuja.
Niruhusu niishi kwa maneno Yako,
nitembee katika njia ing’aayo ya maisha, katika njia ing’aayo ya maisha.
IV
Wajibu wangu nitafanya. Ukarimu Wako nitakulipa.
Nitatumia maisha yangu kwa ajili Yako, nimezaliwa upya ili kukufariji.
Maneno Yako yanaathiri moyo Wangu. Maneno Yako yananitia moyo.
Upendo Wako unaushinda moyo wangu. Katika upande Wako sitaondoka kamwe.
Oo, upande Wako sitaondoka kamwe.
Maneno Yako yanauyeyusha moyo wangu. Mbele Yako nimekuja.
Niruhusu niishi kwa maneno Yako,
nitembee katika njia ing’aayo ya maisha, katika njia ing’aayo ya maisha.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

      Soma zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni