11.19.2018

Mtazamo Ambao Wale Wanaoyatii Mamlaka ya Mungu Wanapaswa Kuumiliki

Mtazamo Ambao Wale Wanaoyatii Mamlaka ya Mungu Wanapaswa Kuumiliki

I
Ni jinsi gani wanadamu wanapaswa kuyajua na kuyastahi
mamlaka ya Mungu, ukuu Wake juu ya kudura ya mwanadamu?
Tatizo hili huwakabili wanadamu wote.
Unapokabiliwa na matatizo katika maisha yako,
utaelewaje na kuonja mamlaka na ukuu wa Mungu? 
Wakati hujui jinsi ya kuyaelewa, kuyashughlikia, na kuyapitia matatizo haya,
ni msimamo gani unafaa kuuchukua ili kuthibitisha
mapenzi yako na hamu ya kuutii mpango wa ukuu wa Mungu?
II
Unapaswa kusubiri mpangilio wa Mungu,
kwa watu, matukio na mambo yaliyopangwa na Mungu,
ukisubiri mapenzi Yake yajidhihirishe yenyewe polepole.
Unapaswa kutafuta kupitia watu na vitu ili kuona jinsi makusudi ya Mungu ni mema,
kuuelewa ukweli Wake na njia ambazo unapaswa kuweka,
kuyaelewa matunda na mafanikio ambayo Anataka kufanikisha kwa wanadamu.
III
Utii na kuukubali ukuu wa Mungu na vitu vyote vilivyowekwa na Yeye,
uje kujua jinsi Muumba anavyoamuru kudura ya mwanadamu,
jinsi Yeye huwakimu wanadamu kwa maisha Yake na kupenyeza ukweli ndani ya mwanadamu.
Vitu vyote huzitii sheria za asili chini ya mpango na ukuu wa Mungu.
Ukiamua kumruhusu Mungu aongoze, kupanga na kuelekeza kila kitu kwa niaba yako,
lazima usubiri, utafute, na kutii.
Mtazamo huu unahitajika na wote wanaosujudu mbele ya Mungu.
Wale ambao hujitahidi kuwa na sifa hii watafikia uhalisi wa kweli.
kutoka kwa "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya


      Soma zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni