2.22.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”


Mwenyezi Mungu anasema, “Wanadamu, walioacha ruzuku ya uzima kutoka kwa mwenye Uweza, hawajui kwa nini wanaishi, na bado wanaogopa kifo. Hukuna usaidizi, hakuna msaada, lakini bado wanadamu wanasita kufumba macho yao, wakiyakabili yote bila woga, wanaendeleza kwa muda mrefu kuishi kwa aibu ulimwenguni humu katika miili isiyokuwa na utambuzi wa nafsi. Unaishi hivyo, pasipo matumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa maumivu na wanatamani sana majilio Yake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote.”

 Tazama zaidi: Filamu za Injili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni