Swahili Gospel Video "Kanisa la Nafsi Tatu ni Mwavuli Wangu"
Wakati mmoja, serikali ya Kikomunisti ya Uchina iliwakamata Wakristo wengi wa Kanisa la Mwenyezi Mungu kutoka mahali fulani usiku wa manane. Jambo hili lilisababisha ghasia kubwa mahali hapo. Lilichochea majadiliano miongoni mwa washirika wa Kanisa la Nafsi Tatu. Watu wengine waliamini kwamba Umeme wa Mashariki umepitia ukandamizaji na mateso ya kikatili ya serikali ya kikomunisti ya Uchina.
Ni hatari sana kuamini katika Umeme wa Mashariki, na ni salama sana kuamini katika Kanisa la Nafsi Tatu. Hawatapitia taabu na wataweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Watu wengine waliamini kwamba Umeme wa Mashariki ndiyo njia ya kweli hasa, lakini mateso na kukamatwa ambayo wanapitia ni makali mno. Kama wangetakiwa kuamini, walifikiri kwamba ni heri kuamini kisiri. Mara serikali ya Kikomunisti ya Uchina ikianguka, wanaweza kuamini kaitka Mwenyezi Mungu waziwazi. Watu wengine walikuwa wemachunguza Umeme wa Mashariki lakini, waliamini kwamba Umeme wa Mashariki unaeneza injili na unashuhudia kwa Bwana bila kujali maisha au kifo na kwamba wanasifiwa na Mungu. Walidhani kwamba watu ambao hujificha ndani ya Kanisa la Nafsi Tatu ni watu waoga ambao wanafuata mkondo maishani bila kusudi na kwamba hawastahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. … Baada ya majadiliano haya makali, je, kila mtu aliweza kujua ni aina gani ya watu wanasifiwa na Bwana na kama waoga wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni?
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni